Wanajeshi wa Marekani wamefanikiwa kumuua kiongozi mmoja wa kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia kupitisha shambulizi la ‘drone’.

Taarifa kutoka Makao Makuu ya Ulinzi wa Marekani (Pentagon) zimeeleza kuwa kiongozi huyo wa Al Shabaab aliyetajwa kwa jina la Hassan Ali Dhoore aliuawa Alhamisi ya wiki hii pamoja na baadhi ya wanamgambo wa kikundi hicho aliokuwa nao katika eneo la Jilib, kusini mwa Somalia, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.

Dhoore anatajwa kuhusika katika kupanga na kufanya mashambulizi ya kigaidi katika uwanja wa ndege wa Mogadishu na hotel moja ya kitalii, mashambulizi ambayo yaliwaua watu takribani 30 wakiwemo raia wa kigeni kutoka nchi mbalimbali pamoja na Marekani. Hivyo, shambulizi hilo ni sehemu ya kulipiza kisasi.

Msemaji wa Pentagon, Peter Cook alisema kuwa walikuwa wakimfuatilia kiongozi huyo na shambulizi hilo lilitekelezwa kumlenga yeye na kufanikiwa. Alisema walichukua siku mbili kabla ya kutangaza tukio hilo kwakuwa walikuwa wanajaribu kuthibitisha matokeo yake.

 

CUF yaivaa China baaa ya kuusifia uchaguzi wa marudio na kutoa msaada
'Bado hatuna Ubavu wa Kukataa misaada, ni kama tumerogwa'