Wakati Rais John Magufuli anawakabidhi Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tausi 25 kila mmoja, ambapo Mama Maria Nyerere amepokea tausi hao kwa niaba ya Baba wa Taifa, amebainisha jinsi ilivyo mlazimu kumfukuza mfanyakazi wa Ikulu aliyezembea kuwatunza Tausi hao.

Akikabidhi tausi hao Rais Magufuli amesema Tanzania haikuwahi kuwa na tausi, lakini waliletwa na Hayati Baba wa Taifa na baadaye Marais wote waliofuata waliwatunza vizuri.

Lakini ilimbidi amfukuze mfanyakazi aliyekuwa anawatunza enzi za uongozi wa Kikwete baada ya kufanya uzembe.

“Nilipoingia pale yule msukuma nikamfukuza kwanza. Kwahiyo, ukija pale huyupo, baadaye tukaleta watalam wa wanyama,” alisema Magufuli.

Kwa upande wake Rais msaafu, Kikwete, ameonesha kushangazwa na maamuzi ya Magufuli baada ya kumfukuza mfanyakazi Msukuma wa Ikulu, ambaye alishindwa kununua incubator ya kutotoa mayai ya Tausi.

“Mimi ndiyo mdogo nasema kwa niaba ya Wazee hawa, tunatoa shukrani kwa moyo wako wa upendo kwa kutupatia hawa ndege, tulikuwa tunawatamani lakini ukitoka nao, ukafika nao Msoga, watu watasema amepora, pia nikupongeze kwa maamuzi ya incubator lakini yule Msukuma sikukuambia umfukuze, lakini nilieleza tu masikitiko yangu,”¬†amesema Dkt Kikwete.

Rais Magufuli alipoingia madarakani alikuta ndege aina ya tausi 403, hadi sasa wameongezeka na kufikia 2,260, na takribani ndege 540 wapo katika Ikulu ya Dodoma.

Polisi wanasa pikipiki 825 zilizoibiwa, waanika mbinu zilizotumiwa na wezi
JPM: Wakulima uzeni mazao kwa bei ya juu, 'Watwangeni kwelikwelI'