Polisi imesema watu wasiofahamika wakiwa na silaha wamewauwa raia 30 katika mashambulizi lililofanywa kwenye vijiji sita kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo hukumbwa mara kwa mara na ghasia za uhalifu na mapigano kati ya jamii.
Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Polisi Jimbo la Sokoto, Ahmad Rufai imeeleza kuwa watu hao, waliuawa na raia waliokuwa wanaendesha pikipiki, huku wakazi kutoka vijiji viwili kati ya vilivyoshambuliwa wamesema waliouawa ni 36.
Wamesema watu hao waliuawa katika mashambulizi ambalo ni la kulipiza kisasi kwa kupinga kulipa pesa za kuwalinda dhidi ya majambazi.
Ghasia za kijamii ni moja ya changamoto za kiusalama zinazomkabili Rais Bola Tinubu, aliyeapishwa wiki iliyopita baada ya kushinda uchaguzi wa mwezi Februari uliogubikwa na tuhuma za wizi wa kura zilizotolewa na vyama vya upinzani.