Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Jackson Kiswaga ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuandaa semina kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Maji na Mazingira, na kutoa wito kwa kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanakuwa endelevu ili kuweza kuwajengea uwezo wabunge.

“Katika hili la Biashara ya Kaboni, naipongeza Serikali kwa hatua hii muhimu tuliyofikia ambayo imelinda zaidi maslahi ya taifa kuhusu rasilimali za misitu. Hapa kwetu square metre moja ni takribani dola 80 ikilinganisha na Marekani ambapo ni Dola 50 kwa square metre moja, hivyo ni jambo la kujipongeza na tunapaswa kuweza mikakati madhubuti ili tuweze kunufaika,” amesema Kiswaga.

Aidha, Kiswaga ambaye ameyasema hayo jijini Dar es Salaam ameiomba Ofisi ya Makamu wa Rais kuweka utaratibu wa usimamizi mahsusi ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaozungukwa na rasilimali zitokanazo na Biashara ya Kaboni ikiwemo misitu wananufaika kupitia miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi itakayoibuliwa na wawekezaji.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Abdallah Hassan Mitawi amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imejipanga kukamilisha utekelezaji wa miradi yote ya mazingira iliyopo pande zote za Muungano ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kunufaika na hivyo kufikia malengo ya miradi hiyo.

Nahodha, Kocha Polisi Tanzania wakubali yaishe
Kesi ya ubadhirifu: Mahakama yamuachilia huru Longondo