Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ameiagiza Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kukifunga kiwanda cha Saruji cha Moshi mpaka mapendekezo yaliyotolewa na Baraza yatakapokamilika.

“Kiwanda hiki kisitishe shughuli za uzalishaji mpaka pale vigezo vya Sheria ya Mazingira vitakapokamili”

Mtambo wa kudhibiti vumbi katika kiwanda cha saruji cha Moshi ambao haufanyi kazi ipasavyo, kumekua na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya uchavuzi wa hewa ufanywao na kiwanda hicho

Makamba amesema hayo katika ziara yake mkoani Kilimanjaro, ambapo akiwa wilayani Rombo ametembelea Kiwanda hicho kufuatia malalamiko ya wananchi juu ya uchafuzi wa hewa itokanayo na vumbi katika shughuli za uzalishaji.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agness Hokororo amesema kuwa Kiwanda hicho kimeendesha shughuli za uzalishaji wa sementi kwa kutofuata sheria ya mazingira ya mwaka 2004 ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mfumo mzuri wa kudhibiti uchafuzi wa vumbi kiwandani hapo.

Aidha, Mratibu wa NEMC Kanda ya Kaskazini, Dkt. Menan Jangu amesema kuwa Ofisi yake ilitembelea kiwanda hicho na kutoa muongozo na taratibu zinazotokiwa kufuatwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.

“Tuliwaelekeza kufanya yafuatayo, kujenga fensi kuzunguka eneo lote la kiwanda, kujenga “pevements” na kuweka mashine maalumu ya kuzuia vumbi kusambaa kwa wingi angani, vitu ambavyo havijafanyiwa kazi.” Alisisitiza Dkt. Jangu

Naye Mwakilishi wa Kiwanda hicho raia wa China, Sophia amesema kuwa suala la kuzungusha uzio eneo lote litatekelezwa pindi hati miliki ya ardhi ya eneo hilo itakapopatikana.

 

Mayanga: Erasto Nyoni Ni Bora Zaidi Ya Kelvin Yondani
Bulgaria Yamponza Danny Blind