Chama cha soka nchini Uholanzi kimetangaza kocha Danny Blind baada ya kufanya nae kazi kwa kipindi cha miaka miwili.

Maamuzi ya kufutwa kazi kwa kocha huyo, yamekuja baada ya kisago cha mabao mawili kwa sifuri walichoambulia Uholanzi katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za kombe la dunia dhidi Bulgaria.

Blind, mwenye umri wa miaka 55, alikabidhiwa jukumu la kuwa kocha mkuu wa Uholanzi, baada ya kuondoka kwa Guus Hiddink mwaka 2015, kufuatia kushindwa kufuzu kwenye fainali za mataifa ya Ulaya zilizofanyika nchini Ufaransa mwaka jana.

Matokeo yanayoandama Uholanzi kwa sasa, yanaiweka nchi hiyo katika mazingira magumu ya kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia za 2018 zitakazofanyika nchini Urusi, japo bado kuna nafasi ya kurekebisha makosa na kuwa sehemu ya timu zitakazotinga kwenye fainali hizo.

Chama cha soka nchini Uholanzi, kimemtua Fred Grim kuwa kocha wa muda wa kikosi cha nchi hiyo, na kazi yake ya kwanza inatarajiwa kuwa kesho ambapo The Orange watacheza dhidi ya mabingwa wa dunia wa mwaka 2006, timu ya taifa ya Italia.

Kiwanda cha Saruji Moshi chafungwa kwa uchafuzi wa mazingira
Video: Kigogo aliyekwenda na Spika bandarini afukuzwa, Bunge lashtuka