Kikosi cha KMC FC hapo kesho kitashuka katika uwanja wa Ilulu hapa mkoani Lindi kwenye mchezo wa mzunguko wa Nne Ligi kuu ya NBC Tanzania bara dhidi ya Namungo utakaochezwa saa 14:00 mchana.

KMC FC ambao ni wageni katika mchezo huo, walifika Lindi Oktoba 20 ambapo jana na leo mchana itafanya maandalizi yake ya mwisho kabla ya mchezo huo wa kesho na kwamba wachezaji , benchi la ufundi wamejiandaa kuhakikisha kwamba kama Timu inapata matokeo mazuri katika mchezo huo.

Maandalizi ya mchezo huo yamefanyika kwa ustadi mkubwa ambapo kila mchezaji anamorali ya kuiwezesha Timu kushinda licha ya kwamba mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na Timu zote mbili kutoka kupoteza mchezo wa mzunguko wa tatu.

Katika michezo mitatu ambayo hadi sasa Timu ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu John Simkoko imeshacheza haijapata matokeo mazuri na kwamba mkakati uliopo ni kujipanga vizuri katika mchezo wa kesho ilikufanikisha adhma ya Timu kupata alama tatu kwani maandalizi yamefanyika vizuri.

“Tunajua tumetoka kupoteza mechi ngumu dhidi ya Yanga, na tunakwenda pia kwenye mchezo mgumu dhidi ya Namungo, lakini hii haitupi hofu na badala yake imetupa changamoto ya kuzidi kupambana hivyo kesho tunaenda kupambania alama tatu muhimu tukiwa ugenini hapa Lindi.”

“Lakini kikubwa tunamshukuru Mungu kwamba wachezaji wote wako salama hakuna mwenye majeraha na kwamba wote wapo tayari kuipambania Timu kwenye mchezo huo ambao kimsingi bado upo ndani ya uwezo wetu kwa maana ya kushinda licha ya ushindani tutakaokutana nao.”

“Tunawashukuru mashabiki zetu kwakuendelea kutusapoti licha ya kuwa hatujakuwa na wakati mzuri tangu kuanza kwa Ligi kuu msimu huu, lakini niwahakikishie tu kwamba ushindi unakuja na tutapanda kwenye nafasi zetu ambazo mmezoea kuiona Timu yetu hivyo hakuna kukata tamaa.” amesema Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC Christina Mwagala

Wabunge wapiga kura kuhalalisha utoaji mimba
Maboresho ya Instagram kunufaisha wengi