Changamoto ambazo bado hazijaanikwa hadharani, zinatajwa kuwa tatizo ndani ya kikosi cha Mbeya City ambacho kimeshindwa kuendelea na moto wa kupata matokeo mazuri, kama ilivyokua mwanzoni mwa msimu huu 2021/22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mbeya City FC jana Alhamis (Juni 16) ilipoteza mchezo tisa msimu huu, kwa kufungwa na Simba SC mabao 3-0, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha Mkuu wa Klabu hiyo yenye maskani yake jijini Mbeya Mathias Lule amesema, kikosi chake kinakabiliwa na changamoto ambazo hakuwa tayari kuzitaja, hali inayopelekea mambo kuwaendea kombo katika ushindani wa Ligi Kuu katika kipindi hiki cha kuelekea ukingoni.

Amesema ni kawaida kwa timu yoyote duniani kupitia changamoto zinazowakabili, hivyo amewataka Waandishi wa Babari na Mashabiki wa klabu hiyo kuelewa kinachowasibu kitapita, na huenda mambo yakawanyookea kwenye michezo iliyosalia.

“Imekua kawaida kwa timu yoyote kupitia changamoto, na sisi ni hivyo, kwa hiyo ifahamike kuwa kuna changamoto zinazotupa matokeo haya, lakini ninaamini mambo yatakua mazuri katika michezo iliyosalia,”

“Hata timu kubwa duniani zimekua na kupanda na kushuka, hivyo hivyo kwa Mbeya City, ndivyo tunavyopata changamoto hizo, kwa hiyo ninaomba nieleweke hivyo, Changamoto ndio sababu.”

Mbeya City iliyoshinda michezo 07, kutoka sare michezo 11 na kupoteza michezo 09, ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 32, imesaliwa na michezo mitatu mkononi.

Sogne amaliza ubishi, Aziz Ki atacheza Young Africans
Matola afichua siri ya kuibanjua Mbeya City