Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Pablo Franco Martin amesema bado anakijenga kikosi chake ili kupata kikosi cha kwanza.

Kocha Pablo ametoa kauli hiyo, baada ya kukishuhudia kikosi chake kikicheza michezo miwili ya ushindani tangu alipokabidhiwa jukumu la kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la Simba SC.

Simba SC iliifunga Ruvu Shooting Mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Ijumaa (Novemba 19) Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kisha ikaichapa Red Arrows Mabao 3-0 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya mtoano.

Kocha huyo kutoka nchini Hispania amesema: “Tunacheza huku tunaitengeneza Simba ya Ushindani, Mpaka sasa ni asilimia 5 tu, Simba ninayoitaka mimi kama kocha, Nadhani baada ya miezi miwili mtaiona Simba ninayoitaka, Nawaambia hakuna timu Afrika itatamani kucheza na Simba Ijayo.”

Kocha Pablo aliajiriwa Simba SC, kufuatia kuondoka kwa Kocha kutoka Ufaransa Didier Gomes mwishoni mwa mwezi Oktoba, baada ya klabu hiyo kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kabla ya mchezo huo Simba SC iliifungwa Jwaneng Galaxy mjini Gaborone-Botswana mabao 2-0.

Matola: Tutafanya mabadiliko ya kikosi
Simba SC kuanza na JKT Tanzania