Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ Simba SC wamepangwa kukutana na Maafande wa JKT Tanzania katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya ASFC msimu huu 2021/22.

Simba SC iliyotwaa ubingwa wa ASFC mkoani Kigoma mwezi Julai mwaka huu kwa kuifunga Young Africans 1-0, imepangwa na maafande hao wanaoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, baada ya kuendeshwa kwa Droo leo Jumanne (Novemba 30), katika studio za Azam TV ambao ni wadhamini wakuu wa michuano hiyo.

Mchezo huo hatua ya 32 Bora ya ASFC umepangwa kuchezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Desemba 15.

wakati Simba SC wakitarajia kuanza na Maafande wa JKt Tanzania, watani zao wa jadi Young Africans wamepangwa kupambana na Ihefu FC katika hatua hiyo ya 32 Bora.

Michezo mingine ya hatua ya 32 Bora baada ya kuendeshwa kwa Droo leo Jumanne (Novemba 30).

Kocha Simba SC awatuliza mashabiki
Waziri Bashungwa awaagiza BASATA kumsaidia Mzee Stima