Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ Moses Basena amesifu kiwango kizuri kilichoonyeshwa na mastaa wa Taifa Stars akisema licha ya kupoteza mbele yao, lakini kuna vipaji vipya ambavyo kama vitashikiliwa vitaipaisha nchi kimataifa miaka michache ijayo.

Kocha huyo aliyewahi kuinoa Simba SC alisema soka la Tanzania linazidi kupiga hatua kila siku kutokana na wachezaji wengi kupata nafasi ya kucheza nje ya mipaka ya nchi yao.

“Wachezaji kama Simon Msuva, Novatus Dismas na wengine wengi wameonyesha wana kitu kikubwa sana kwa nchi huko mbeleni kwani ukiwaangalia unaona ni kizazi bora kinachokuja, soka la sasa linategemea vijana na ili upige hatua ni lazima uwaandae huko mbeleni.” amesema Basena

“Kwenye timu ni lazima uwe na wazoefu na hata kwetu unaona tunamtumia bado, Emmanuel Okwi lengo ni kutengeneza muunganiko na vijana ili wazidi kujifuza zaidi kutoka kwao,” amesema.

Basena anamsaidia Milutin Sredojevic ‘Micho’ baada ya Charles Livingstone Mbabazi kuitema timu hiyo kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi, huku akiwana kumbukumbu ya kunoa Simba SC mwaka 2011 japo kwa muda mfupi.

PICHA: Young Africans yaondoka Dar es salaam
Papa Francis apata maradhi ya kupumua, alazwa