Saa chache kabla ya kuanza safari ya kuifuata TP Mazembe nyumbani kwao Lubumbashi-DR Congo Kocha Mkuu wa Young Africans  amesema, wataingia kwenye mchezo huo wa mwisho wa Kundi D, Kombe la Shirikisho kwa nidhamu kubwa ili kupata matokeo mazuri.

Young Africans itacheza mchezo huo katika Uwanja wa TP Mazembe Jumapili (April 02), huku ikiwa na tiketi ya kucheza Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika, baada ya kuifunga US Monastir ya Tunisia Machi 19, jijini Dar es salaam.

Akizungumza kabla ya safari ya kuelekea Lubumbashi, DR Congo mapema leo Alhamis (Machi 30) Kocha Nabi amesema ni muhimu kwa mchezo ujao kucheza kwa umakini, huku wakijiwekea lengo la kupata ushindi ugenini.

“Tumefurahi kwa kufanikisha malengo ya timu kufuzu hatua ya Robo Fainali, bado kuna malengo yanapaswa kuendelea kutimia ikiwa ni pamoja na ushindi mchezo wetu ujao.”

“Ambacho tunakifanya kwa sasa ni jitihada kwenye maandalizi na kuwakabili wapinzani kwa nidhamu kubwa jambo litakalotupa matokeo mazuri ugenini,”

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam Februari 19, Young Africans iliifunga TP Mazembe mabao 3-1.

Young Africans ina alama 10 kwenye Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kucheza michezo mitano, ikiongoza Kundi D, sawa na US Monastir ya Tunisia.

TP Mazembe inaburusa mkia wa Kundi hilo ikiwa na alama 03, ikitanguliwana AS Real Bamako ya Mali yenye alama 05.

Azam FC yahamishia nguvu ASFC
Robertinho: Tutaiheshimu Raja Casablanca