Kikosi cha Young Africans kimeondoka leo Alhamis (Machi 30) kwenda jijini Lubumbashi, DR Congo kwa ajili ya kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe utakayopigwa Jumapili (Aprili 02).

Young Africans ambayo ipo kileleni mwa Kundi D inasaka rekodi ya kumaliza hatua ya makundi ikiwa nafasi hiyo ambayo ina faida ya kuanzia ugenini mchezo wa Robo Fainali na kumalizia ugenini uwanja wa Benjamin Mkapa.

Young Africans itahitaji ushindi mnono ambao utawafanya US Monastir inayocheza na AS Real Bamako isiufikie ili kujihakikishia nafasi hiyo.

Waziri Bashungwa azindua Bodi Shirika la Mzinga
Kocha The Cranes aitabiria makubwa Taifa Stars