Kaka wa kiungo wa klabu ya Man City, Yaya Toure (Kolo Toure) amesema bado anaamini ndugu yake anaweza kubaki na Man city, licha ya kuhusishwa na taarifa za kuwa kwenye mipango ya kuondoka Etihad Stadium mwishoni mwa msimu huu.

Kolo Toure, amezungumza jambo hilo, ambalo linakinzana na wakala wa ndugu yake aitwaye Dimitri Seluk, ambaye anapenda kuona Yaya akiwa ni mwenye furaha wakati wote.

Kolo amesema suala la Yaya kuondoka Man City bado halina nafasi kwa sasa kutokana na mustakabali wake kuwa wazi, na anaamini wakati wowote viongozi wa klabu hiyo watalizungumza na litamalizika.

Kolo ambaye anaitumikia klabu ya Liverpool, amefichua siri nyingine kwa kusema alizungumza na nduguye siku mbili zilizopita na alimueleza kwamba mchezo kati ya Man city dhidi ya PSG, ungefanya maamuzi ya mustakabali wake, na kwa sasa anaamini mambo yatakaa sawa kutoka na  matajiri hao wa mjini Manchester kupata ushindi wa jumla wa mabao matatu kwa mawili.

Hata hivyo amekiri kuwepo kwa maelewano hafifu kati ya ndugu yake na Pep Guardiola ambaye atakabidhiwa kikosi cha Man City mwishoni mwa msimu huu, lakini akasisitiza kuwa na imani suala hilo litamalizika.

Wakala wa Yaya, amekua akishiniza suala la mchezaji wake kushughulikiwa kwa haraka kwa kupatiwa mkataba mpya ili afahamu mustakabali wake klabuni hapo, ambapo tayari imeanza kuelezwa huenda kiungo huyo kutoka nchini Ivory Coast akakosa nafasi chini ya utalawa na meneja mpya Pep Guardiola.

 

Sakata la Ufisadi wa Mabilioni ya Jeshi la Polisi lageuka kaa la moto
Misri Waanza Kujiandaa Na Mchezo Wa Mwezi Juni Dhidi Ya Stars