Mkataba wa kusambaza mashine za kutambua alama za vidole ulioingiwa kati ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises wenye thaamni ya shilingi bilioni 37 umegeuka kuwa kaa la moto.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeagiza kwa barua jeshi hilo kuwasilisha nyaraka za mkataba huo ndani ya siku tatu kuanzia siku ambayo barua yao imepokelewa na Ofisi ya Bunge.

Agizo hilo limetolewa baada ya wiki iliyopita kutoa Kamati hiyo kutoa siku 7  kwa Jeshi hilo kuwasilisha mkataba huo ambao ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ya Mwaka 2013/14 ilibaini kuwa Jeshi hilo lilisaini mkataba wa shilingi bilioni 37 na kampuni ya Lugumi kwa ajili ya kusambaza mashine hizo katika vituo 408, lakini ni vituo 14 tu vya polisi vilivowekewa mashine hizo wakati kampuni hiyo ilishapokea asilimia 90 ya malipo.

Ukomo wa siku 7 ulikamilika juzi ambapo Kamati hiyo ilidai hadi jana ilikuwa haijapokea taarifa za mkataba huo kama ilivyoagiza.

Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Aeshi Hilaly aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Kamati hiyo imechukua hatua ya kuliandikia barua Jeshi hilo kutokana na kuonesha kukaidi agizo la kwanza walilolitoa mwa maneno.

“Siku zote tumekuwa tukitoa maagizo kwa mdomo na taasisi nyingi zimekuwa zikitekeleza, lakini hili la mkataba wa Lugumi naona kwa wenzetu limekuwa gumu, hivyo tumeamua kuwakumbusha kwa maandishi,” alisema.

Arsenal Kumuweka Sokoni Aaron James Ramsey
Kolo Toure: Yaya Atabaki Man City Msimu Ujao