Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba amewataka wakazi wa wilaya hiyo kujikinga na maabukizi ya virusi vya Ukimwi ambapo ametaja takwimu ya watu walijitokeza kupima VVU ambapo wanaume ni 437 na wanawake ni  375 huku 62 wakibainika kuwa  na maambukizi ya VVU.

Ameyasema hayo leo Octoba 10, 2021 wakati akitoa taarifa ya upimaji  virusi kwenye mkesha wa mwenge wa uhuru mjini Ushirombo.

Hata hivyo wakazi hao wamepewa kondomu 1,666 ili kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya  Ukimwi (VVU).

Nkumba amesema katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru wananchi walichagiajia damu na kuchanja chanjo ya Uviko -19 watu 4.

Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Luteni Josephine Mwambashi amewataka wananchi kuendelea kujikinga na maambukizi mapya VVU.

Zaidi ya watu Laki Nane wamepata Chanjo ya UVIKO-19 Nchini Tanzania
Kuna jambo: Taliban, Marekani wajifungia Qatar