Taarifa iliyotolewa na Majeshi ya Korea Kusini na Japan imesema kuwa Korea Kaskazini imerusha kombora moja la balastiki ndani ya maji kwenye pwani ya Japan, hali hiyo imejitokeza wakati wakuu wa ujasusi wa Korea Kusini, Japan na Marekaini wameripotiwa kukutana huko Seoul kujadili Korea Kaskazini.

Aidha Katika wiki za hivi karibuni, Pyongyang imeanza majaribio kadhaa ya kile inachodai kuwa ni makombora ya kusafiri kwa masafa marefu, na silaha za kupambana na ndege.

Siku ya Jumanne Wakuu wa jeshi la Korea Kusini walisema kombora moja lilizinduliwa kutoka bandari ya Sinpo, mashariki mwa Korea Kaskazini ambapo Pyongyang kawaida huweka manowari zake. Ilitua katika Bahari ya Mashariki, pia inayojulikana kama Bahari ya Japani.

Waziri Mkuu wa Japani Fumio Kishida amesema kulikuwa na makombora mawili ya balistiki.

Korea Kaskazini imeendelea mbele na majaribio yake ya makombora kwani Korea Kusini pia inaunda silaha zake, kwa kile waangalizi wanasema kimegeuka kuwa mashindano ya kujikusanyia silaha kwenye peninsula ya Korea.

Waziri Gwajima awafungua macho diaspora
"YE" ndilo jina jipya la Kanye West