Mgombea wa Urais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ally Mwinyi amewaahidi wazanzibar kuwa endapo atapata ridhaa ya kuwaongoza atawashughulikia wabadhirifu wa mali za umma na wale wote watakao haribu matarajio ya ujenzi wa nchi.
“Wapo wanaodhani upole wangu ni udhaifu leo nataka niwaambie ipo siku watanielewa tutakuwa wakali sana kwa watu ambao hawaendani na matarajio ya yetu ya ujenzi wa uchumi mpya kwa manufaa ya nchi yetu”. amesema Mwinyi.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni leo Septemba 12, Mwinyi amehainisha mambo watakayo yavalia njuga kwenye serikali ya awamu ya nane ikiwemo kukuza uchumi wa bahari kwa kupanua wigo wa utalii, kukuza sekta ya uvuvi wa wa bahari kuu na ufugaji wa samaki hii itakuza fursa ya ajira.
Amesema mafuta na gesi ni kipaombele pia, miundo mbinu bora, barabara zenye viwango vya rami urefu wa kilomita 198kwa unguja na pemba, kuboresha huduma za jamii, na kuendeleza utoaji wa elimu bure na kuongeza udahili katika shule zote mpaka vyuo vikuu.
Vipaombele vingine ni utekelezaji wa miradi ya maji, kukuza viwanda, kukuza ajira na kilimo cha mboga na matunda.