Serikali ya Kenya, imesema haitafumbia macho vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyopangwa na wapinzani wake, katika wakati ambapo Muungano wa kisiasa wa Azimio unaoongozwa na Raila Odinga, ukipanga kufanya maandamano na mkutano wa kisiasa.

Onyo hilo limetolewa na Rais wa Kenya, William Ruto, ikiwa ni muendelezo wa majuma kadhaa ya rais Ruto na wapinzani wake kurushiana maneno kuhusu matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana (2022), yaliyompa ushindi.

Rais wa Kenya, William Ruto.

Ruro amesema, “msiwe na wasiwasi hii Kenya tutaiunganisha iwe kitu kimoja, mimi siwezi ruhusu watu wachache watupangie njama ya kututisha ha hili nalisema kwa moyo mmoja hatutavumilia hali hiyo kwa namna yoyote.”

Vyama vya upinzani nchini Kenya, vimekuwa vikidai kuwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana yaliratibiwa na vimeahidi kutoa ushahidi na kuweka nguvu madai yao ili hatua stahiki dhidi ya suala hilo zichukuliwe.

Mwanasiasa maarufu auawa kwa risasi na wasiojulikana
Thierry Henry: Ten Hag ana mwaka mmoja Man Utd