Jana, Septemba 20 ilikuwa siku ya furaha kwa familia ya Diamond Platinumz na mashabiki wake waliposherehekea siku ya 40 ya mtoto wake ‘Tiffah’ tangu alipozaliwa.

Sherehe hiyo pia iliambatana na kuoneshwa hadharani kwa mara ya kwanza kwa mtoto huyo ambaye amekuwa maarufu na milionea akiwa bado mchanga.

Kumekuwepo na taarifa mbalimbali kuwa kuna kiasi cha fedha ambacho kimewekwa na Diamond Platinumz kwa ajili ya watu ambao wangependa kumuona Tiffah uso kwa uso.

Tiffah2

Hata hivyo, Diamond Platinumz ameiambia BBC kuwa taarifa hizo ni za uongo na kwamba hakuna gharama yoyote ambayo mtu anapaswa kulipia kwa kumuona mtoto huyo ambaye picha yake ya kwanza inayoonesha sura yake hadharani ilidhaminiwa na benki kubwa nchini.

Katika hatua nyingine, Diamond alieleza sababu zilizopelekea kumfungulia binti yake huyo akaunti ya Instagram tangu akiwa tumboni.

“Ulimwengu wa mitandao sasa hivi, ulimwengu unakua na unavyomkuza mwanao lazima umtengeneze mapema, umtengenezee mazingira ya kuwa brand mapema hususan sisi watu maarufu. Na namshukuru Mwenyezi Mungu tangu siku aliyozaliwa hadi sasa hivi siku zinavyozidi kwenda anazidi kuingiza [pesa]. Ni mtu anayeingiza hela japokuwa hajaanza kuwa na ufahamu wake,” Diamond aliiambia BBC.

Hans Poppe: Yanga Jiandaeni Kunywa Supu
Kwa Nini Mrembo Wako Anaweza ‘Kukusaliti’ Ingawa Anaonesha Ana Msimamo?