Baada ya chanzo kimoja kuthibitisha Ijumaa iliyopita kuwa Kylie Jenner ameachana na mpenzi wake rapa Tyga baada ya kutofautiana, mrembo huyo amechochea kuni kwa kuweka vielelezo kadhaa.

Kupitia Instagram, Kylie ameweka vipande vya video kadhaa vikimuonesha akifuatisha kwa mdomo (lip sync) nyimbo zenye mashairi yanayoonesha kutafuta faraja kwa mtu aliyeachwa.

Katika vipande hivyo, Kylie anaonekana akifuatishwa sehemu ya mashairi ya wimbo wa Bryson Tiller ‘Been That Way’. Mashairi hayo yanasema, “I wanna know how we became so distant, girl’.

Katika kipande kingine, Kylie anafuatisha wimbo wa Bryson Tiller ‘Overtime’, katika sehemu ya mashairi inaesema “I feel it, you hurting and I’ve been healing”.

 

Magufuli Aagiza Mamilioni Ya Kumpongeza Yakanunue Vitanda Muhimbili
Picha: Lil Ommy wa Times Fm Afanya Ziara Redio Kubwa Za Afrika Kusini, Aeleza Ulichojifunza