Lil Ommy ndani ya Studio

Lil Ommy ndani ya Studio Afrika Kusini

Mtangazaji wa Kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm, Omary Tambwe maarufu kama Lil Ommy yuko Johannesburg nchini Afrika Kusini ambapo ameenda kufanya ziara binafsi yenye lengo la kujifunza na kupata uzoefu zaidi nchini humo.

Lil Ommy akiwa katika kituo cha SABC

Lil Ommy akiwa katika kituo cha SABC

Lil Ommy ameeleza kuwa aliamua kuanya ziara hiyo kwa kuwa anataka kuongeza uzoefu zaidi na kujifunza mambo ambayo nchi za Afrika zilizoendelea zinafanya katika vituo vyake vya radio na jinsi vipindi vinavyotayarishwa na kufikishwa kwa wasikilizaji.

Moja kati ya vitu alivyojifunza, ni pamoja na utaratibu usioruhusu upendeleo wa aina yoyote kutokana na matakwa binafsi ya mtangazaji katika upigaji wa nyimbo. Pia, heshima ya wasanii kwa vipindi husika.

“Huwezi kuweka studio ukakuta show iko hewani ukaichezea tu lazima usubiri muda wako ufike ufanye, hata kama ni msanii gani muda wake inabidi awepo na ukifika interview itaanza on time labda kuwe na jambo kubwa la kitaifa. Huwezi kucheza muziki nje ya rotation iliyopo hata kama ni msanii gani. Ngoma yake itasubiri mpaka ipite process zote ndo iende,” ameongeza.

Lil Ommy ameeleza kuwa tofauti na ilivyo Tanzania ambapo watangazaji wengi wanatamani kuchanganya kiingereza kwenye vipindi vyao, watangazaji wa Afrika Kusini ingawa hawazungumzi Kiswahili lakini wanakipa thamani kubwa sana.

“Jamaa wana promote zaidi muziki wao na lugha yao kwenye redio wanachanganya Zulu, wanapenda kujifunza Kiswahili, wanaichukulia kama lugha kubwa ya bara la Afrika ukiachana na Kiingereza kuwa lugha ya kimataifa.”

Kylie Jenner achochea Kuni Taarifa za Kupigana Chini na Tyga
Forbes: Mo Dewji aongoza Kwa Utajiri Tanzania, Dangote Aendelea Kuishika Afrika, Orodha Kamili