Jarida la Forbes kupitia toleo lao la ‘50 Africa’s Richest People’ limetoa orodha ya watu wenye utajiri mkubwa zaidi barani Afrika huku Aliko Dangote akiendelea kushika nafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa $16.6 bilioni.

Aliko-Dangote1

Katika orodha hiyo, Mohamed Dewji ameshika nafasi ya kwanza nchini Tanzania huku akiwa katika nafasi ya 21 Afrika akiwa na utajiri wa $1.1 Bilioni hivyo kuingia kwenye orodha ya mabilionea. Kwa Tanzania, Dewji anafuatiwa na Rostam Aziz mwenye utajiri wa $900 milioni.

Mwaka jana, Dewji ambaye ni mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya METL aliahidi kuendelea kumfukuzia Aliko Dangote na kwamba ajiandae kumpisha katika nafasi hiyo ya kwanza.
Forbes
forbes6

Picha: Lil Ommy wa Times Fm Afanya Ziara Redio Kubwa Za Afrika Kusini, Aeleza Ulichojifunza
Magufuli: Nimejipa Kazi Ya Kuwa Mtumbua Jipu