Mwanamitindo na mfanyabiasha maarufu nchini Marekani Kylie Jenner ametumia neno la kiswahili ‘Hakuna matata’ aliloambatanisha na picha, lugha hii adhimu inaendelea kukua siku hadi siku.

Kama ilivyo kwenye filamu ya ‘Lion King’ ambayo ameshiriki mwanamuziki maarufu Beyonce, Donald Glover na wengine neno hili limetumika pia, sambamba na hayo neno kama ‘Uishi kwa muda mrefu Mfalme” limetumika mwanzoni mwa wimbo wa ”Spirit” ambao umetumika kama Sound track ya filamu hiyo.

Lugha ama maneno ya kiswahili kutumika na wasanii au watu mashuhuri wa ughaibuni haijaanza leo, ikumbukwe mwaka 1987 Micheal Jackson aliimba ”Nakupenda pia nakutaka pia mpenzi wee” kwenye wimbo wake ujulikanao kama Liberian Girls.

Hata hivyo baadhi ya watu maarufu waliomba nyimbo zao na kutumia Lugha adhimi ya kiswahili ni pamoja na Boney M aliye imba wimbo wa ”Malaika”  mwaka 1981 Miriam Makeba alipoimba hiyo hiyo ‘Malaika” mapema mwaka 1974.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 16, 2019
LIVE MWANZA: Rais Magufuli katika uzinduzi wa huduma za tiba hospitali ya Rufaa Bugando

Comments

comments