Aliyekua rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF, Lamine Diack amejiuzulu wadhifa wake kama mwanachama wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC.

Diack alisimamishwa kwa muda na IOC, kutokana na tuhuma za kupokea hongo ili kuwaficha wanariadha waliogundulika wametumia dawa za kusisimua misuli, wakati akiwa rais wa IAAF.

Mwanzoni mwa juma hili, IAAF ilihusishwa na tuhuma za kuchangia katika matumizi ya dawa za kusisimua misuli kwenye ripoti ya shirika la kukabiliana na matumizi ya dawa hizo duniani Wada, na hapo ndipo msisitizo wa kujiuzulu kwa kiongozi huyo ulipotolewa.

Mwanae Diack, Papa Massata, mshauri wake Habib Cisse na mkuu wa zamani wa kukabiliana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli IAAF Gabriel Dolle pia wanachunguzwa na maafisa wa polisi wa nchini Ufaransa.

Kwa mujibu wa viongozi wa mashtaka nchini Ufaransa, Diack anashutumiwa kupokea pesa kwa lengo la kuficha ukweli dhidi ya wanariadha kadhaa wa nchini Urusi ambao walikua na hatia ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku mwaka 2011, kabla ya maandalizio ya michuano ya Olimpiki.

Hata hivyo wanariadha hao, watachukuliwa hatua za kinidhamu na IAAF, kutokana na ukweli wa vipimo vyaoa mbao ulikua umefichwa kwa makusudi binafsi.

Diack mwenye umri wa miaka 82, alifikisha kikomo uongozi wake wa miaka 16 katika IAAF mwezi Agosti, huku Mwingereza Coe, mshindi mara mbili wa Olimpiki mbio za 1500m, akichaguliwa kuchukua nafasi yake.

Blatter Yu Hoi Hispitalini
Gabon, Sudan Zakwama Kombe La Dunia 2018