Beki kutoka nchini Ufaransa, Laurent Koscielny amesisitiza mchezo wao kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uholanzi unapaswa kuchezwa mwishoni mwa juma hili, licha ya mashambulio ya kigaidi kutokea mjini Brussels nchini Ubelgiji hapo jana

Watu 34 walipoteza maisha kufuatia mashambuliaji hayo yaliyotokana na milipuko katika uwanja wa ndege wa Zavantem pamoja na kituo cha treni cha Maalbeek Metro.

Tukio hilo limetokea, ikiwa ni baada ya miezi minne kupita ambapo Ufaransa waliwapoteza watu 130, kufuatia shambulio la kigaidi la jijini Paris.

Koscielny, amesema anatambua kila mmoja ameguswa na tukio hilo la mjini Brussels lakini hakuna budi kwa mchezo wao na Uholanzi kuchezwa kama ulivyokua umepangwa.

Amesema tayari wameshatuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Ublegiji na anaamini huo ni mchango mzuri kwa wachezaji wa Ufaransa ambao pia umewagusa wengine wanaoishi nchini humo.

Hata hivyo amekumbushia kwamba wakati shambulio la kigaidi likitokea jijini Paris mwezi Novemba mwaka 2015, timu yao ya taifa ilicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya England siku iliyofuata, hivyo hata mchezo wao wa juma hili unapaswa kuendelea.

Wakati Koscielny, akitoa msisitizo wa mchezo wao na Uholanzi kuchezwa siku ya ijumaa, viongozi wa shirikisho la soka la Ufaransa FFF, hawajasema chochote licha ya hali ya ulinzi kuimarishwa katika sehemu zote za nchini humo.

Marekebisho Ya Ratiba Ya Vodacom Premiership
Novak Djokovicn Akubalia Yaishe