Kinara wa ubora katika tennis duniani upande wa wanaume, Novak Djokovic, ameomba radhi kufuatia kauli yake ya kutaka washiriki wa kiume kulipwa zawadi maradufu zaidi ya wanawake, aliyoitoa mwishoni mwa juma lililopita mara baada ya michuano ya Indian Wells Masters huko nchini Marekani.

Djikovic, amewasilisha radhi zake kwa mashabiki kupitia mitandao ya kijamii, ambapo katika kurasa zake za Twitter na Facebook ziliandikwa maneno ambayo yalionyesha anajutia kauli yake.

Maneno aliyoaandika gwiji huyo wa tennis katika mitandao hiyo ya kijamii, yalisomeka: “Sikua na maana mbaya kama ilivyopolekea kutoakana na kauli niliyoizungumza mwishoni mwa juma lililopita, lakini sina budi kuomba radhi”.

Bingwa huyo mara 11 wa Grand Slam, alizungumza kauli hiyo baada ya kushinda mchezo wake wa hatua ya fainali dhidi ya Milos Raonic, na alionekana alikua hafahamu athari ya kitakachotokea baadae.

Laurent Koscielny Ashauri Mtanange Wa Ufaransa Upigwe
Wekundu Wa Msimbazi Na Hadithi Za Kususia Michezo Ya Ligi