Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umetishia kujitoa katika ushiriki wa Ligi kuu soka Tanzania bara endapo Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF litaendelea hatu a za kutojibu na kutoshughulikia malalamiko yao mbalimbali waliyowapelekea.

Suala hilo limekuja baada ya klabu hiyo kuiandikia barua TFF ya kulalamikia kuvurugika kwa ratiba ya ligi kuu soka Tanzania bara hasa madai ya kuwepo kwa viporo vingi kwa klabu za Yanga na Azam Fc ambazo zinashiriki mashindano ya kimataifa hivi sasa.

Akizungumza mara baada ya kupeleka barua ya kulalamikia madai hayo katika makao makuu ya TFF yaliyopo karume jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara amesema wameamua kufanya hivyo baada ya kuona mara nyingi TFF ikisena haijapokea barua kutoka kwao.

Manara amesema barua yao kwenda kwenye kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo wameitaka TFF kuanza kufanyia kazi malamiko yao na kufatilia Kesi zote walizowapeleka ikiwemo kesi ya Ramadhani Singano kuelekea Azam fc,kesi ya Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma kumpiga kichwa mchezaji wao Hassan Kessy,kesi ya Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha klabu ya Yanga Jerry Muro kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya klabu ya Simba.

Novak Djokovicn Akubalia Yaishe
UEFA: Ufaransa Itakua Salama Wasalmin