Wakati Rais John Magufuli akitangaza kuanza kutekeleza ahadi yake ya elimu bure kuanzia Januari 2016, aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amehoji namna ya utekelezaji wa ahadi hiyo.

Lowassa amemtaka Rais Magufuli kufafanua ahadi yake kama itawagusa tu wanafunzi ambao wataanza masomo Januari mwakani au hata wale ambao wako shuleni hivi sasa.

Aliwataka wananchi kutofautisha kati ya utekelezaji wa ahadi ya elimu bure wa Rais Magufuli na elimu bure aliyoiahidi yeye na chama chake cha Chadema.

“Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu, serikali yetu ingegharamia. Na nilitangaza kufuta michango mashuleni ili kumpunguzia mwananchi mzigo,” alisema Lowassa.

Alisema kuwa Rais Magufuli ameagiza watendaji wa serikali kuhakikisha elimu bure hadi kidato cha nne inaanza kutolewa Januari mwakani lakini alimtaka kueleza wazi endapo ahadi hiyo itawagusa pia wanafunzi wanaendelea na masomo.

Katika hatua nyingine, Lowassa alieleza kuwa suala la mikopo ya elimu ya juu kwake lisingekuwa tatizo kwani alikuwa ameahidi kutoa elimu bure hadi chuo kikuu.

Alisema kuwa hivi sasa wanafunzi wanahangaika na mikopo na kwamba amesikia kuwa kati ya wanafunzi 70,000 ni asilimia 17 pekee ndio waliopewa mikopo.

 

 

Malinzi Kuzindua Rasmi Kombe La Shirikisho
FA Kumuadhibu Tena Jose Mourinho?