Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema kuwa kwa sasa anafanya siasa za kimataifa  zaidi huku akiwataka wananachi kufanya kazi kwa bidii  kwa kuwa hatua ya Donald Trump kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani Dunia imebadilika.

Ameyasema hayo wakati wa ibaada maalum ya shukrani na kuuombea mwaka mpya wa 2017 iliyoshirikisha madhehebu mawili ya kanisa Katoliki na lile la KKKT usharika wa Monduli.

Lowassa amesema kuwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump ni mwamba asiyetabirika hivyo ni vyema kila mmoja akajikita kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuwa huyo wa taifa la kubwa ulimwenguni hakubaliani na wa aina yoyote.

“Dunia imebadilika, amechaguliwa Rais mmoja huko Marekani, mwamba kweli kweli,hatuwezi kumtabiri mambo yake yatakavyokuwa,lakini tukubaliane kila mtu afanye kazi kwa bidii na kwa maarifa ni mhimu sana hakubali upuuzi wowote”amesema Lowassa.

Aidha, Lowassa amewataka  Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro na mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isaac Joseph kuhakikisha miradi inayopitishwa inawanufaisha wananchi kwa asilimia mia moja.

Tulia: Tanzania mpya inawezekana
Rais Magufuli amtumbua Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco