Leo Mei, 23, 2018 katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad anatarajia kuwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kufanya mahojiano na waandishi wa habari juu ya mambo mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii pamoja na kutoa ufafanuzi wa kina juu ya mwenendo wa Chama chake cha CUF.

Ziara hiyo ni kufuatia mualiko alioupata kutaka kwa Muungano wa Klabu ya waandishi wa Habari Tanzania (Union Of Tanzania Press Club-UTPC) ambao ni waandaaji wa kipindi cha ”Tujadiliane” kinacholenga kufanya mahojiano na watu mbalimbali wakiwemo viongozi na wafanyakazi wa Serikali na Taasisi binafsi.

Aidha mahojiano hayo yataendeshwa na Emmanuel Bulendu na kurushwa mubashara katika mitandao ya kijamii ya Facebook katika ukurasa wa Julius Mtatiro, pia  yatasikika katika Radio Sauti, RFA, KISS FM, Afya Radio, Metro FM, Radio Sengerema, HSC, Living Water, Ukombozi FC, Iqra FM, na Kwa Neema Radio.

Katika ziara hiyo, Maalim Seif ataongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Mbarala Maharagande na kupokelewa na Wanachama pamoja na viongozi wa CUF wa ngazi mbalimbali za Chama jijini humo.

 

Rooney kutimkia Marekani
Babu Tale akabiliwa na shtaka zito, apandishwa kizimbani