Imefahamika kuwa hatua ya kutimuliwa kwa aliyekua meneja wa kikosi cha AC Milan, Sinisa Mihajlovic ilipewa msukumo mkubwa sana na rais wa klabu hiyo Silvio Berlusconi.

Berlusconi, alifanya maamuzi hayo kwa kutumia nguvu ya kuwa mtu wa mwisho kutoa maamuzi ya kiutendaji, baada ya kuchoshwa na mwenendo wa Mihajlovic ambaye alioneonekana kushindwa kuliendesha jahazi la kikosi chake.

Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya uongozi wa AC Milan zinaelza kwamba, Berlusconi alishauriwa kwa ukaribu na mshauri wake Arrigo Sacchi pamoja na mtendaji mkuu wa klabu Adriano Galliani, juu ya kutochukua maamuzi ya kumfuta kazi meneja huyo kutoka nchini Serbia, lakini ilishindikana.

Viongozi hao wawili walimtaka rais wa AC Milan kufanya subra na kuendelea na Mihajlovic hadi mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuona wameshashindwa kufikia malengo waliokua wamejiwekea, lakini ushauri huo ulikua mgumu.

Mbali na kushauriwa hivyo pia Berlusconi, alitahadharishwa juu ya utendaji wa kazi wa meneja wa muda Cristian Brocchi, kutokana na kutokua na uzoefu na mikiki mikiki ya ligi ya nchini Italia (Sirie A) ambayo kwa sasa inaelekea mwishoni mwa msimu.

Cristian Brocchi alitangazwa kuwa meneja wa muda wa AC Milan hapo jana, ikiwa ni dakika chache baada ya maamuzi ya kufutwa kazi kwa Mihajlovic kufanywa na kikao cha wakuu wa klabu hiyo ya mjini Milan.

Brocchi amepandishwa hadi kwenye kikosi cha wakubwa akitokea katika kikosi cha vijana kama kocha mkuu.

DUKA LA DAWA LAJENGWA NDANI YA HOSPITALI RUANGWA
Arsenal Kumuweka Sokoni Aaron James Ramsey