Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Kenya cha ODM, Raila Odinga amesitisha maamndamano yaliopangwa kufanyika Jumatatu ya leo Aprili 3, 2023 baada ya Rais William Ruto kuhutubia taifa na kumtaka Odinga kutaka wakae chini kuzungumzia tofauti zilizopo.

Rais Ruto, ambaye alikuwa akihutubia taifa Ikulu jijini Nairobi, alitoa kauli hiyo wito wa ushirikiano wa pande mbili Bungeni, kuhusu kuundwa upya kwa (IEBC), kama moja ya jambo linalolalamikiwa na kuchangia uwepo wa maandamano ya kuipinga Serikali.

Ruto kupitia hotuba hiyo amesema, “ninapendekeza ushirikiano wa pande mbili Bungeni kuhusu uundaji upya wa jopo la Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi – IEBC ndani ya vigezo vya sheria na katiba inayotambulika.”

Kwa upande wake Raila amebainisha kuwa wameamua kusitisha maandamano haya ya Jumatatu na Alhamisi wiki hii, ili kuruhusu mazungumzo kuhusu masuala yaliyoibuliwa akisema, “tuko tayari kushiriki na tutajihusisha bila aina yoyote ya rushwa na mchakato huu unapaswa kuanza mapema kesho.”

Odinga pamoja na viongozi wa Azimio waliibua maswala mazito ikiwa ni pamoja na gharama ya maisha , suala la uteuzi wa makamishana wa IEBC , ukosefu wa uwazi katika mfumo wa uchaguzi, na idara ya usalama kutumia nguvu kupita kiasi katika kukabili wanadamanaji ambapo watu 10 wakiwemo maafisa wa polisi wakipoteza maisha.

Waarabu wanaziwinda Simba SC, Young Africans CAF
Ibenge bado yupo sana Al Hilal Omdurman