Maandamano ya kuiunga mkono serikali ya Iran yamefanyika jijini Tehran Ijumaa huku uongozi wa nchi hiyo ukitaka kuyamaliza machafuko yaliyotokea wiki iliyopita.

Maandamano hayo yamejiri mara baada ya Marekani kuiwekea vikwazo Iran na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha kikao maalum kuizungumzia hali hiyo.

Aidha, mapema hii leo katika barabara za Tehran kulikuwa na idadi kubwa ya maafisa wa polisi ingawa hakukuwa na ripoti za maandamano mapya usiku kucha, lakini zimekuwepo taarifa kwamba kulikuwa na maandamano madogo madogo ya kuipinga serikali katika miji mbalimbali.

Hata hivyo, Wanaharakati wameweka video katika mitandao ya kijamii kuonyesha maandamano hayo ambapo wamesema kuwa waandamanaji walikuwa wanatamka maneno ya kumpinga kiongozi Ayatollah Ali Khamenei.

 

Droo ya raundi ya tatu kombe la shirikisho
Majaliwa ahimiza kilimo cha Kahawa