Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri kwa kumuhamisha aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa kuwa Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo Februari 14, 2023 ambapo aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amehamishiwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Dkt. Hassan Abbas sasa amekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Katika mabadiliko mengine, Rais Samia pia amemuhamishia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii akichukua anachukua nafasi ya Profesa Eliamani M. Sedoyeka.

Dkt. Samia pia amemteua Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, akichukua nafasi ya Dkt. Hassan Abbas, ambapo kabla ya uteuzi huo, Yakub alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

TAKUKURU yabaini upotevu Laki 3.8 za makusanyo kila siku Stendi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 15, 2023