Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Mkoani Dodoma, imebaini upotevu wa wastani wa shilingi 380,000 kwa siku katika makusanyo ya mapato, ambayo ni sawa na zaidi ya Shilingi milioni 11 kwa mwezi, fedha ambazo zingeweza kutumika katika miradi ya kimaendeleo.

Hayo yamebainika baada ya kutolewa kwa taarifa ya utendaji kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha Oktoba – Desemba 2022 na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dodoma, Sosthenes Kibwengo mbele ya Waandishi wa Habari hii leo Februari 15, 2023, huku ikiarifiwa kuwa baadhi ya maeneo hakuna kabisa taarifa za makusanyo wala matumizi, na Wananchi kutokatiwi risiti baada ya kulipa ushuru.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dodoma, Sosthenes Kibwengo.

Amesema, “kuna usimamizi duni wa kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa mfano wakati tunafuatilia katika eneo moja tumekuta kuna upotevu wa wastani wa shilingi 380,000 kwa siku katika makusanyo ya mapato hizi ni fedha nyingi zaidi ya milioni 11 kwa mwezi.”

Aidha, amesema katika kuikabili hali hiyo wameona ni vyema kuibainisha na kuziba mianya ya rushwa na tayari wamefanya warsha 11 katika sekta za Afya, Manunuzi, Fedha, Ardhi, Biashara, Kilimo na Mifugo ambapo maazimio yalifikiwa na muda wa utekelezaji kuwekwa.

Kampeni huduma msaada wa Kisheria Mama Samia yazinduliwa
Mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri