Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewataka Watendaji wa Kata na Viongozi wa Mikoa wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), kutumia vitendea kazi wanavyokabidhiwa na serikali katika kuwafikia wananchi kwa urahisi, kuwasikiliza, kuwahudumia na kufuatilia miradi ya maendeleo.

Sehemu ya Magari 54 ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji
Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Dkt. Mpango ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, katika hafla iliofanyika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma eneo la Mtumba hii leo Februari 14, 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akihutubia Viongozi na Watumishi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 54 kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Hafla iliofanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma – Mtumba hii leo Februari 14, 2023.

Amesema, Maafisa watendaji wanatakiwa kutambua na kushughulikia changamoto za wananchi kwa kuhakikisha vikao katika ngazi ya Vijiji na Mitaa vinafanyika kama inavyopaswa huku akiwaasa kuacha uzembe katika usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli nyingine za kijamii.

Sehemu ya Magari 54 yaliyotolewa kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).

Aidha, Dkt Mpango pia amesema ni muhimu kuzingatia uhifadhi wa mazingira kwa kutoa hamasa kwa wananchi ili wawe mstari wa mbele katika shughuli za uhifadhi ikiwemo kupanda miti na usafi wa mazingira ili kuwepo na maendeleo endelevu.

Familia ya marehemu 'AKA' yarudi na tamko hili jipya
Habari Picha: Utiaji saini mikataba 26 Gridi imara