Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Songwe kuchunguza mtumishi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Silas Meshilieki pamoja na fundi Seremala Michael Bangu kwa tuhuma za kuchukua mbao zilizokamatwa na samani na kuzipeleka kwa fundi Bangu kinyume na taratibu za uhifadhi.

Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi, madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Songwe akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Songwe na kusema mbao hizo zilizokamatwa na kupelekwa kwa fundi Bangu kinyume na taratibu za uhifadhi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Awali, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde alisema Rais Dkt. Samia anataka matokeo chanya katika utendaji na ana imani kubwa na watumishi wa umma, hivyo wafanye kazi kwa bidii, ili wasimuangushe.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alisema tayari Serikali imeshakamilisha usanifu wa mradi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Mbalizi-Changombe-Mkwajuni-Saza-Patamela-Makongorosi yenye urefu wa kilomita 118 na kuwataka waendelee kuwa na subira.

Wanaodaiwa kuwa Panya Road wakamatwa na Polisi
Halmashauri zatakiwa kubuni miradi mikubwa