Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu sita wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu maarufu kama Panya Road walishikwa wakiwa na baadhi ya vitu mbalimbali walivyoiba, ikiwemo simu.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watu hao wamekamatwa wakati wa operesheni maalum inayoendelea katika maeneo ya Bunju A na Bunju B na mapinga, Bgamoyo Mpakani.

Watuhumiwa matukio mbalimbali ya uhalifu wakishuka ndani ya gari la Polisi.

“Nitoe onyo Panya Road hawa wakijitoa ufahamu wakajaribu kushambulia Askari Polisi, Polisi watajihami na watajihami kwa kutumia nguvu inayolingana na mashambulizi na aina silaha wanazozitumia,” amesema Kamanda Muriro.

Kamanda Muliro amesema, watuhumiwa hao sita mbali na kukamatwa pia wanadaiwa kufanya vitendo mbalimbali vya uhalifu, na kusema Polisi haitawavumilia wale wote watakaobainika kuvunja amani na utulivu.

Habari Picha: Utiaji saini mikataba 26 Gridi imara
Fundi Seremala aliyeishika sharubu Serikali akalia kuti kavu