Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amelizungumzia lengo la Kampeni ya Kitaifa ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, kuwa ni kuimarisha upatikanaji wa haki kwa Umma.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo hii leo Februari 15, 2022 wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kampeni hiyo pia inalenga kuimarisha utoaji wa msaada wa kisheria kwa umma.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro katika uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.

Amesema, “kwa kutumia jitihada za kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hasa haki za wanawake pia tunalenga kuimarisha huduma ya ushauri wa kisheria na unasihi kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.”

Kampeni ya Kitaifa ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia itatekelezwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa ushirikiano wa Wizara zenye dhamana, Taasisi za Kiserikali, Mashirika yanayotoa msaada wa kisheria na wadau wa maendeleo ya jamii.

Uhalifu: Kamishna awakutanisha Watendaji, Polisi Kata
TAKUKURU yabaini upotevu Laki 3.8 za makusanyo kila siku Stendi