Kikosi cha Ujasusi, Ofisi ya Ujasusi, Garki cha jijini Abuja kimemuweka kizuizini Mchungaji Kiongozi wa House on the Rock Abuja, Mchungaji Uche Aigbe, kwa kuhubiri huki akiwa amebeba Silaha aina ya AK-47 akiwa madhabahuni.

Inadaiwa kuwa, Kamishna wa Polisi, Kamandi ya Jimbo Kuu la Shirikisho, Sadiq Abubakar, alitoa pendekezo kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Usman Baba, kumfukuza kazi afisa wa polisi, Inspekta Musa Audu anayedaiwa kumpatia mchungaji huyo silaha.

Mchungaji Kiongozi wa House on the Rock Abuja, Mchungaji Uche Aigbe.

Tayari Polisi wa nchini humo wameanza uchunguzi kuhusu tukio hilo, baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha Mchungaji huyo akiwa amebeba Bunduki hiyo inayodaiwa kuwa ni ya Inspekta mmoja wa Polisi, Musa Audu .

Inspekta Audu, anaweza kukakabiliwa na kesi ya utaratibu ya kukabidhi bunduki yake kwa Mchungaji Kiongozi wa House on the Rock, Abuja Chapter, Uche Aigbe, siku ya Jumapili Februari 12, 2023.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 15, 2023
Familia ya marehemu 'AKA' yarudi na tamko hili jipya