Baadhi ya mabalozi wa Marekani wamekuwa wakitafuta njia za ubunifu za kuonyesha uungaji mkono wao kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja LGBTQ pamoja na mwezi wa kujivunia walivyo-Pride month -baada ya Ikulu ya Marekani, White House kupiga marufuku kupeperushwa kwa bendera yao ya rangi saba za upinde wa mvua.
Kabla ya mwaka huu 2019 balozi zote za Marekani zilikuwa zinapeperusha bendela ya wapenzi wa jinsia moja lakini mwaka huu walitakiwa kuomba idhini kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo ambayo iliripotiwa kukataa kutoa idhini hiyo.
Jumanne ya wiki hii, makamu wa rais wa nchi hiyo, Mike Pence alisema kuwa uzuiaji huo wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo ilikuwa ni sahihi na ni uamuzi unaofaa lakini hakuna masharti yaliyowekwa dhidi ya bendera za wapenzi wa jinsia moja kupeperushwa kwenye majengo mengine.
Aidha, utawala waRais wa nchi hiyo, Donald Trump uliwateuwa baadhi ya mabalozi ambao wanafahamika kuwa ni wapenzi wa jinsia moja na Trump alitoa taarifa akisherehekea mwezi wa kujivunia wa mapenzi ya jinsia moja.
“Tunajivunia kwa kuweza kumtumikia kila Mmarekani, lakini linapokuja suala la bendera ya Marekani katika balozi za Marekani na miji mikuu yote kote duniani, ni bendera moja tu ya Marekani inayopeperushwa,” amesema MikePence
Katika hatua nyingine, Mike Pence, ambaye ni muhubiri wa Kikristo , anapinga ndoa za wapenzi wa jinsia moja na ana historia ya kuunga mkono kupingwa kwa sheria ya mapenzi ya jinsia moja.
Hata hivyo, wapenzi wa jinsia moja wanasherekea mwezi wa kujivunia walivyo-Pride month, ambapo balozi mbalimbali za Marekani duniani kote zimekuwa zikipeperusha bendera ya wapenzi wa jinsia moja wakiashiria kuunga mkono huku baadhi ya mabalozi wa nchi hiyo yenye nguvu duniani wakifahamika kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.