Katika safari ya kutetea ubingwa wa kombe la klabu bingwa barani Afrika, klabu ya TP Mazembe kutoka Jamuhuri Ya Kimokrasia Ya Congo itakutana na mabingwa kutoka Morocco Wydad Casablanca kwenye raundi ya pili ya mtoano ya Kombe la klabu bingwa Afrika mwaka huu.

TP Mazembe ilifanikiwa kukata tiketi ya kushiriki raundi hiyo baada ya kuitoa St. George SC inayonolewa na Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mart Noij kwa jumla ya mabao 3-2.

Huku wapinzani wao Wydada Casablanca walifanikiwa kutinga raundi hiyo ya pili baada ya kuwanyuka mabingwa wa nchini Madagascar CNaPS Sport kwa jumla ya mabao 6-3.

Manny Pacquiao apigwa marufuku hii Marekani
Majaliwa aeleza siri ya Magufuli kuteua Wakuu wa Mikoa Majenerali wa Jeshi