Kampuni ya MacLeans BeneCIBO Limited inayo jihusisha na usambazaji wa vyakula vya mboga mboga na matunda imeanzisha utaratibu maalumu wa kununua mazao ya wakulima wilayani lushoto mkoani Tanga moja kwa moja kutoka shambani.
Hatua ambayo itamnufaisha mkulima kwa kuinua kipato chake na kuwa na uhakika wa soko la mazao yake hasa yanayoharibika haraka Kama mboga mboga na Matunda kwani mkulima hatahitaji kumtumia dalali tena.
Nnala Mwakanyamale mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo amesema kuwa wameamua kuanza ukusanyaji wa mboga na matunda kwa wakulima wa lushoto mkoani Tanga, na kuyahifadhi katika vyumba maalum vya baridi na kusafirisha hadi jijini Dar es salaam, ili mkulima ajue thamani yake na kuboresha maisha yake.
Kwa upande wa Daktari wa mimea, Kimomwe Halifa ambaye amekuwa anafanya kazi kwa ukaribu na wakulima wilayani lushoto mkoani Tanga amesema kuwa hatua ya kampuni ya MacLeans BeneCIBO kununua mazao kutoka kwa wakulima shambani ataleta mapinduzi ya kilimo hasa Cha mbogamboga na matunda wilayani humo.
Aidha licha ya kununua mazao, wakulima watapata nafasi ya kupata mikopo midogo midogo kutoka kampuni ya Kopafasta bila riba.
Hata hivyo, MacLeans BeneCIBO imelenga kuinua maisha ya wakulima nchi nzima na kuboresha maisha ya walaji kwa kupata chakula kilichoandaliwa kwenye mazingira yaliyo Bora kwa kauli mbiu ya chakula bora kwa afya bora.