Watendaji wa Madawati ya Jinsia ndani ya jeshi la Polisi nchini wametakiwa kujiepusha na tabia za kutoa siri za waliopitia vitendo vya ukatili wa kijinsia hali inayosababisha wananchi kushindwa
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Jumanne Sagini alisema jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha watendaji wa madawati ya jinsia na watoto nchini.
Naibu Waziri Sagini amesema kuwa, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wateja ambao wamekuwa wakipeleka malalamiko katika Jeshi hilo na kueleza kuwa Askari wanaofanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo.
Kwa upande wake Kamishna wa Kamisheni ya Polisi jamii ,CP Faustine Shilogile ameeleza njia mbalimbali ambazo Jeshi hilo linatumia katika kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu ya ukatili dhidi ya watoto na wanawake pamoja na kupinga mila potofu.
Aidha, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto nchini Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Maria Nzuki ameeleza changamoto mbalimbali ambazo zinakabili ofisi za dawati la jinsia nchini ikiwemo uchache wa majengo ya uendeshaji dawati hilo, ukosefu wa vyombo vya usafiri ili kuwawezesha kuwafikia waathirikia wa matukio ya ukatili wa kijinsia.