Lengo la sanaa ni kufikisha ujumbe kwa hadhira lengo likiwa kuburudisha, kuonya au kukosoa vile vile kuelimisha na ndivyo baadhi ya wasanii wanaofanya vizuri kwenye sanaa hufanya.

Roma Mkatoliki ameonekana kama msanii ambaye anaburudisha huku akikumbusha majukumu ya viongozi kupitia nyimbo zake pendwa huku wakati mwingine akiilenga serikali moja kwa moja

Baada ya kuachia wimbo wake mpya wiki iliyopita ”Kaa tayari” umeonekana ujumbe umewafikia walengwa  na ndio maana hoja za ujumbe uliokuwa umemlenga Meneja wa Tip Top connection na Diamond Platnumz zikiwa hazikatiki.

Boss kamganda Dangote kaisahau Tip Top ni moja ya mstari ambao umekua ukiibua hoja huku msanii kutoka kundi la Tip Top, Madee jana katika ukurasa wake wa twita alichangia hoja kuhusu wimbo huo .

babu-tale

”tumeusikia wimbo wa @roma Mkatoliki kama una ukweli wowote thn tutawajibu” Madee

madee

Mkubwa Fella ambaye pia ni Meneja wa TMK na kituo cha Mkubwa na wanae pamoja na Diamond Platnumz wiki iliyopita alionekana kukubaliana na kauli ya Roma kuhusu Tale kuiacha Tip Top na kwamba waliambiana wafanye kazi lakini wasisahau kundi la TMK pamoja na Tip Top.

“Unajua Roma ni mtu mzima, alichoimba hata mtaani huko watu wanasema, na unaweza kuona labda Roma ameambiwa hayo maneno na msanii kama Madee au msanii mwingine yeyote wa kwetu, lakini hata mimi nilishawahi kumwambia mdogo wangu Babu Tale kuwa tufanye yote lakini yeye asiisahau Tip Top Connection na mimi nisiisahau TMK,” Fella alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.

Mashirika Ya Kidini Kuimalisha Mahusiano na Serikali Katika Utendaji Kazi
Mguu Sawa: Profesa Jay arudi kivingine na mchanganyiko wa Singeli