Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph ‘Profesa Jay’ Haule amewaweka mguu sawa mashabiki wake kupokea audio na video ya wimbo wake wa kwanza tangu achaguliwe kuwa mbunge.

Profesa Jay 3

Profesa Jay ameonesha kuchanganya ladha ya Hip hop na Singeli kwa kumshirikisha msanii maarufu wa Singeli, Sholo Mwamba katika wimbo wake huo alioupa jina la ‘Kazi Kazi’.

Jana, rapa huyo alifika katika eneo la Uwanja wa Fisi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushoot video ya wimbo huo inayoongozwa na Travellah.

“Kazi kazi video shooting. Kwa heshima kubwa sana tumeshoot video hii maeneo ya Manzese – Uwanja wa Fisi Tukiwapa tumaini jipya na nguvu wale wote waliokata tamaa na kuwaambia wakomae kwa kufanya kazi ipo siku mambo yatakuwa sawa. Kazi kazi . Professor Jay Featuring Sholo Mwamba,” aliandika Profesa Jay na kuipamba akaunti yake kwa picha za tukio hilo.

Profesa Jay 2

 

Madee Aonesha Kuguswa na Ujumbe wa Roma Kuhusu 'Tip Top' Kutekelezwa
Ukimya wa Msanii Hamisi Amani Kujibiwa leo Mchana