Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka madiwani wa Manispaa ya Tabora kutojihusisha na biashara ya aina yoyote zinazotolewa na Ofisi ya Mkurugezi na wametakiwa kubaki kuwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
Ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na Madiwani, Watumishi wa Manispaa, watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Watendaji wa ngazi mbali mbali wa taasisi za umma zilizopo Manispaa ya Tabora ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake mkoani humo.
Amewataka Madiwani ambao wanajihusisha na Kampuni zinazofanya biashara na Halmashauri ya Manispaa hiyo wajiondoe ili waweze kuchukua hatua pale inapotokea tatizo au dosari yoyote.
Aidha, Majaliwa ametolea mfano wa mradi wa ununuzi wa Magari mawili na kontena za kubebea taka ambao alipewa mmoja wa madiwani wa Manispaa hiyo ambaye hakumtaja jina, huku akisema kuwa kampuni hiyo ilinunua magari hayo huku moja likiwa bovu.
-
Wakuu wa wilaya watakiwa kufanya tathmini kwenye halmashauri zao
-
BREAKING: Rais Magufuli akiongea na Wananchi Sengerema
-
Habari Picha: Rais Dkt. Magufuli amjulia hali Dada yake aliyelazwa hosptali ya Bugando
Kwa upande Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bosco Ndunguru amesema kuwa ni kweli kampuni hiyo ilileta gari moja likiwa ni bovu lakini malipo yake bado hawajamlipa hadi hapo atakapoleta gari jipya.