Mashabiki wa bondia Manny Pacquiao wamepatwa na mshtuko baada ya Rais wa Ufilipino, Benigno Aquino III kueleza kuwa taarifa za kiintelijensia zimebaini kuwa magaidi wa kundi la Abu Sayyaf wana mpango wa kumteka mbabe huyo wa ndodi.

Rais Benigno Aquino III amesema kuwa Magaidi hao ambao walimuua na kumkata kichwa John Ridsdel Jumatatu ya wiki hii, walikuwa na mpango wa kumteka Manny Pacquiao pamoja na kumuua Rais huyo.

Alisema kuwa mpango wa kumteka Manny Pacquiao ulikuwa umejikita katika hatua zao za kujipatia fedha kutoka kutoka Serikalini pamoja na kuungwa mkono kwa kupata fedha kutoka katika kundi la ISIS.

Mbali na mpango huo, Rais wa Ufilipino alieleza kuwa magaidi hao walifanya shambulizi kubwa la bomu katikati ya jiji la Manila.

 Baadhi ya wanamgambo wanaounda kundi la kigaidi la Abu Sayyaf

Hata hivyo, mipango yao ilibainika na kuvurugwa na vyombo vy asalama kabla hawajaanza utekelezaji.

Rais Aquiano ambaye kipindi chake cha uongozi kinamalizika mwezi Juni mwaka huu amewahakikishia wananchi wa Ufilipino kuwa atahakikisha analidhoofisha kadri iwezekanavyo kundi hilo la kigaidi.

Korea kuwapa Tanzania Walimu wa Hisabati na Sayansi kupunguza uhaba
Wabunge watakiwa kulipwa kutokana na wanavyochangia mijadala, wapinzani wapiga ‘kimya’