Rais John Magufuli anajiandaa kupokea majukumu mazito ya kukiongoza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Dk. Jakaya Kikwete, muda wowote.

Hayo yameelezwa na msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka wakati akielezea yaliyojiri katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika wiki hii, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, chini ya mwenyekiti wake, Dk. Kikwete ambapo Rais John Magufuli pia alihudhuria.

Ole Sendeka amesema kwamba ingawa kipindi cha uenyekiti ni miaka mitano, kama ilivyo kwa marais waliopita, Dk. Kikwete ameamua kumpa kijiti hicho Dk. Magufuli mwaka huu.

“Mwaka huu wakubwa hawa walishashauriana, Kikwete alishatangaza wazi kwamba anakusudia kumkabidhi nafasi ya uenyekiti Rais wa sasa, Dk. Magufuli wakati wowote mwaka huu na kinachofanyika sasa ni maandalizi .

Alisema kuwa maandalizi yakikamilika muda wowote chama hicho kitatangaza tarehe ya kufanyika kwa makabidhiano hayo. Rais Magufuli atakuwa na jukumu la kukiongoza chama hicho na kuhakikisha kinaibuka na ushindi katika uchaguzi ujao.

Uchaguzi Wa Young Africans Wapigwa Kalenda
IGP Mangu atoa masharti ya kumpandisha cheo trafiki aliyepambana na mke wa waziri